NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, October 16, 2012

Mwanamke wa kwanza kuongoza AU

 
Aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma ameapishwa kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika.
Dr Dlamini-Zuma mke wa zamani wa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni mwanamke wa kwanza kabisa kushika wadhifa huo.
Akiwa kama mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika ataongoza juhudi za kutatua baadhi ya matatizo sugu barani Afrika ikiwemo mgogoro wa Mali na ule wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, na pia hatari ya kutokea vita kati ya Sudan na Sudan Kusini.
Akiwa mwanasiasa wa muda mrefu nchini Afrika Kusini Dr Dlamini-Zuma aliwahi kuwa waziri wa afya, mambo ya ndani na pia waziri wa mambo ya nje.
1
Nkosazana akipongezwa baada ya kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa tume ya Umoja wa afrika


No comments:

Post a Comment