NJOMBE

NJOMBE

clock

Saturday, October 6, 2012

Mabilioni ya faida kwa Samsung

Kampuni ya simu ya Samsung, imesema inatarajia kupata faida kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha kati ya mwezi Julai hadi Sepetemba.
Kampuni hiyo inasema faida zake zimetokana na mauzo yake ya simu za Galaxy Smartphone.
Aidha Samsung inasema inatarajia kuwa na faida ya dola bilioni saba.
Faida hiyo ni mara dufu ya faida iliyopata mwaka jana na pia iko juu zaidi ikilinganishwa na kile wadadisi walikuwa wametabiri.
Hata hivyo,wadadisi wanasema kuwa mvutano wa kisheria unaoendelea kati ya kampuni hiyo na ile ye Apple, unaleta wasiwasi kuhusu mustakabali wa kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment