NJOMBE

NJOMBE

Wednesday, October 24, 2012

HIVI, UNA TATIZO LA KUSHIKWA NA HASIRA HADI KUFIKIA HATUA YA KUDHURU WENGINE? SOMA HAPA NJIA ZA KUEPUKA HILO.

Najua kila mmoja wetu kuna kipindi,
 anapatwa na hasira 
pale ambapo anaona ameendewa 
kinyume na alichotarajia.
Inawezekana 
ni ofisini,
 nyumbani, 
au hata njiani hali hii ikakukuta.

Je, 
kupatwa na hasira ni upungufu wa
 afya ya akili?
Jibu ni hapana,
hasira huwa zipo na zimeumbwa kwa kila binadamu.
Kwahiyo kushikwa na hasira ni jambo la kawaida ila kutenda jambo baya la kumdhuru mtu au mali kutokana na hasira huo ni upungufu.
Kila mmoja wetu,
 anatakiwa awe makini katika kuzitawala hasira zake na aweze kujizuia pale 
anapoona zimezidi.

Hebu tuangalie njia saba zinazoweza kukusaidia kuzitawala hasira zako:

1.ONDOKA ENEO HILO

Kama upo mazingira fulani
 na ukaudhiwa 
na hasira kali ikakushika,
ondoka kwa dakika chache eneo hilo na ukafikirie vizuri.
Ukifanya hivi,
 unasaidia kupunguza uzito wa yaliyokufanya uchukie 
kwani ubongo utapata nafasi ya 
kutafakari upya.

2.ELEZEA HASIRA YAKO UKIWA NA UTULIVU

Unapoelezea,
 hasira yako kwa mtu/watu 
waliokufanya ukasirike unasaidia 
kupunguza uzito wa 
tukio moyoni mwako.
Elezea kwanini
 ulichukia na kwa utulivu kabisa bila kumuumiza mtu mwengine 
kwa maneno yako omba 
lisirudiwe tena.

3.FANYA MAZOEZI

Mazoezi ya viungo 
yanasaidia kupunguza hisia kali 
moyoni mwako pale 
zinapotaka kuripuka.
Kama unaona una hasira nzito, 
nenda eneo la mazoezi 
anza kufanya mazoezi ya kukimbia au 
kama una chumba cha mazoezi 
kwako ingia anza kufanya mazoezi na utaona mabadiliko yake.

4.FIKIRIA KABLA HUJAZUNGUMZA

Ukiwa ushapamba moto wa hasira, 
ni rahisi
 kuzungumza maneno makali ambayo 
yanaweza yakashusha utu wako au wa unayemwambia.
Chukua dakika chache,
 kutafakari
 maneno ya kutumia na uone kama hayatokuharibia au kumuharibia mwengine heshima yake.

5.FIKIRIA SULUHISHO MBADALA

Badala ya kuendelea kutafakari
 kilichokufanya uchukie,
anza kufikiria namna ya kutatua tatizo lililojitokeza 
kati yako na upande wa pili.
Yawezekana mtoto wako anaharibu vitu hovyo,
dereva wako anachelewa 
kukufuata eneo unalomtaarifu,
au mpenzi wako anachelewa kufika eneo la miadi.
Fikiria suluhisho mbadala kwani tukio 
baada hasira linaweza likaifanya 
hali kuwa mbaya zaidi.

6.USILIMBIKIZE MATUKIO 

Kusamehe matukio yaliyopita 
na kuyasahau 
ni njia inayopunguza uzito wa 
tukio jipya.
Ukisamehe watu waliokukosea utakuwa umejisaidia mwenyewe na 
wao pia kujifunza kitu kutokana 
na tukio hilo.
Kwani usitarajie binadamu mwenzako awe
 vile vile 
unavyotaka na kutamani wewe awe.

7.TAFUTA MSAADA

Jinsi ya kuzuia 
hasira ni
 changamoto kwa kila binadamu,
kwani ukishindwa kuzizuia na 
ukachukua uamuzi mbaya unawaumiza watu wanaokuzunguka.
Kwa hiyo chagua mtu wako ambaye utakuwa unaenda kuomba msaada wa ushauri 
kutokana na 
tukio lililokuudhi.

KUKASIRIKA SI DHAMBI 
ILA INAONYESHA KUWA AKILI YAKO 
INA AFYA YA KUJUA KIPI HUPENDI NA KIPI UNAPENDA KUFANYIWA.

LAKINI 
UNATAKIWA UZITAWALE HASIRA 
PALE UNAPOONA ZITAKUPELEKA KATIKA KUFANYA TUKIO BAYA DHIDI YA MWENGINE.

No comments:

Post a Comment