NJOMBE

NJOMBE

Sunday, October 14, 2012

VURUGU MBAGALA, JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATU KADHAA KUFUATIA VURUGU ZA WAISLAMU MBAGALA

Jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Temeke jijini Dar es salaam, linawashikilia watu kadhaa kufuatia vurugu zilizofanywa na waumini wa dini ya kiislamu hapo jana maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam kufuatia waumini hao kufanya uharibifu mkubwa katika makanisa mbalimbali yaliyopo eneo hilo ikiwa ni kuonyesha hasira zao kufuatia kijana wa miaka 14 anayefahamika kwa jina la Emanuel Josephat kukojolea kitabu cha msahafu(Quran) wakitaniana na rafiki yake.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Temeke David Misime ameiambia Wapo Radio Fm kuwa licha ya kuwashikilia watu hao bado wanaendelea kufanya msako wa kuwakamata watu wengine zaidi kutokana na tukio hilo la uvunjifu amani. Mpaka sasa makanisa yamepata uharibifu kutokana na tukio hilo ambayo ni Kanisa la Assemblies of God, Lutheran, Wasabato, Anglican yote ya maeneo hayo ambako vioo milangoni vilivunjwa, gari kuchomwa, vyombo kuharibiwa na kuchomwa moto.
 

 Kwa upande wa sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhaji Musa Salum amewataka viongozi kutoka misikiti yote jijini kuwaeleza waumini wao kutopandikiza chuki kwa dini nyingine hali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa,'' Wakristo wasihukumiwe kutokana na tukio hilo, kwani aliyefanya hivyo ni mtoto akiwa katika utani na mwenzake ...hajatumwa na kanisa, ni watoto waliofanya hivyo na jazba isiwepo kabisa'', alisema sheikh Salum.
Hamis Salum baba mzazi wa kijana aliyekojolea kitabu hicho
Ameongeza kuwa hata kipindi cha mtume, tukio kama hilo la mtu kukojolea msikitini liliwahi kutokea na waumini kutaka kumdhuru, lakini walikatazwa kutokana na imani kutoruhusu adhabu kama hiyo. Hivyo aliwataka waislamu wote kutulia katika kipindi hiki na kuacha jazba kutokana na kijana aliyefanya tukio hilo kushikiliwa na polisi.


Moja ya gari lililovunjwa kioo.
Chanzo cha Habari Gospel Kitaa

No comments:

Post a Comment