NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, October 23, 2012

Mahakama ya Norway yasikiliza kesi za Rwanda


Mahakama za Gacaca zilisika baadi ya kesi za mauaji ya kimbari nchini Rwanda
Mahakama ya Norway imeanza kusikiliza mashahidi katika kesi dhidi ya Bwana Sadi Bugingo, raia wa Rwanda anayeshtakiwa kwa makosa ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Mashahidi wanasikilizwa na mahakama hiyo wakiwa mjini Kigali kwa kutumia teknolojia ya video.
Hii ni kesi ya kwanza ya mauaji ya kimbari ya Rwanda kusikilizwa na nchi ya Norway.
Mwandishi wa BBC mjini Kigali Yves Buchana, anasema kuwa mashahidi 3 wamesikilizwa na mahakama hiyo ya mjini Oslo wakiwa katika chumba cha mahakama nchini Rwanda.
Mashahidi wawili waliotangulia walikuwa wa upande wa utetezi wa Bwana Sadi Bugingo.Wote wamesikika wakisema kuwa wanamfahamu kama mfanyabiashara aliyekuwa anasaidia watu wala hawamfahamu katika vitendo vya uhalifu.
shahidi wa pili mwanamke kutoka kabila la watutsi ambaye amesema ni shemeji wa mtuhumiwa huyo amesema kuwa wakati wa mauaji ya kimbari Sadi Bugingo aliwahi kuwasaidia walipovamiwa na kundi la wanamgambo likitaka kuwaua akafanikiwa kulishawishi lisiwauwe.
Jumla ya mashahidi 70 wanatarajiwa kusikilizwa baadi wakiwa wa upande wa utetezi wengine wakiwa dhidi ya mshukiwa.Buchana anasema kuwa mashahidi wanaulizwa maswali na upande wa mashtaka na upande wa utetezi kwa kutumia teknolojia ya video.
Sadi Bugingo mwenye umri wa miaka 47 alikuwa mfanyabiashara na mwenye ushawishi mkubwa katika wilaya ya Ngoma mkoa wa mashariki ambako inadaiwa alifanyia makosa wakati wa mauaji ya kimbari.
Rwanda inamtuhumu kuhusika na mauaji ya kimbari,uhalifu wa kivita kuhamasisha mauaji hayo na kuunda genge la wahalifu.Hii ni kesi ya kwanza kusikilizwa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda na mahakama ya Norway ,hatua ambayo imepongezwa na Rwanda licha ya kwamba serikali ilikuwa imeomba kukabidhiwa mtuhumiwa huyo.

No comments:

Post a Comment