NJOMBE

NJOMBE

Friday, October 5, 2012

Tutu bingwa wa kupigania uhuru

Askofu mkuu mstaafu Desmond Tutu
Mwanaharakati mashuhuri dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Askofu Desmond Tutu, amekabidhiwa tuzo maalum yenye thamani ya dola za kimarekani milioni moja kutoka taasisi moja inayopigania utawala bora barani Afrika.
Wakati ikikabidhi zawadi hiyo taasisi hiyo ya Mo Ibrahim Foundation imemuelezea Askofu Tutu kama mmoja wa sauti muhimu kupigania uhuru barani Afrika.
Imesema bwana Tutu aliyewahi pia kupewa tuzo ya amani ametumia maisha yake yote kupigania haki na demokrasia.
Wakfu huo wenye makao yake mjini London,unasifika kwa kuwatuza wanaharakati mashuhuri na kutoa tuzo ya dola milioni tano kila mwaka kwa rais mmoja wa zamani ambaye alisifika kwa uongozi wake bora.
Tuzo hiyo imetolewa mara tatu katika miaka yake saba tangu kuzinduliwa.

No comments:

Post a Comment