NJOMBE

NJOMBE

Friday, October 12, 2012

Kampuni ya Shell mahakamani Uholanzi


Eneo la Niger Delta lina barabara chache na vijiji vingi havina umeme wala maji safi
Waakilishi wa kampuni kubwa ya mafuta ya Shell, wamefika mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kuchafua mazingira nchini Nigeria.
Wakulima wanne kutoka eneo lililo na utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta nchini Nigeria leo wameifikisha Kampuni hiyo kubwa ya mafuta ya Shell katika mahakama ya kimataifa ya uholanzi kujibu madai ya uchafuzi wa mzingira katika vijiji vinne nchini Nigeria.
Kesi hiyo ni moja kati kesi ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na vyombo mbali mbali vya habari duniani. Ikiwa wakulima hao watashinda kesi hiyo, huenda ikatoa nafasi kwa maelfu ya watu wanaodai fidia kutoka kwa makampuni kama Shell.
Wakulima hao wanasema uvujaji wa mabomba ya mafuta yanayomilikiwa na kampuni hiyo yameharibu mashamba yao na biashara ya samaki.
Wa-Nigeria hao wakiungwa mkono na wanaharakati wa mazingira kutoka Uholanzi wanataka Kampuni ya Shell ilazimishwe kusafisha mazingira na kulipa fidia kwa hasara iliyotokea huko Niger Delta.
Kesi hiyo imewasilishwa mahakamani na wakulima wanne wa Nigeria kwa ushirikiano na shirika moja la kutetea mazingira la nchini humo, Friends of the Earth.
Ni mara ya kwanza kwa kampuni kubwa ya Uholanzi inashtakiwa katika mahakama ya kiraia nchini humo kuhusiana na uharibifu uliotokea katika nchi ya kigeni.
Shell, inasisitiza kuwa haijaweza kusafisha eneo ambalo lilichafuka kutokana na shughuli zake nchini Nigeria.
Inasemekana kuwa nusu ya uvujaji wa mafuta katika eneo hilo umesababishwa na visa vya wizi.
Kesi hiyo inahusishwa na uvujaji wa mafuta uliotokea katika eneo la Ogoniland nchini Nigeria.
Wakulima wanasema kuwa mafuta yaliyovuja kutoka kwa mabomba ya mafuta ya kampuni hiyo, yameathiri mapato yao, kwa kuharibu mimea na mabwawa ya samaki.
Mmoja wa walioshtaki kampuni hiyo, Alfred Akpan, aliambia BBC kuwa mafuta yaliyovuja yaliharibu vibaya mabwawa yake 47 ya samaki na anataka fidia.

No comments:

Post a Comment