NJOMBE

NJOMBE

Saturday, March 31, 2012

TAASISI YA HASSAN MAAJAR TRUST YAANZISHA DUKA LA HISANI MIKOCHENI

 Mjumbe wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Zuhura Sinare Murro akizungumza katika uzinduzi wa duka la hisani la taasisi ya Hassan Maajar Trust uliofanyika kwenye jengo la Arcade Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo duka hilo linauza vifaa mbalimbali zikiwemo ngua za kiume, nguo za kike, viatu N.K.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Zena Maajar Tenga akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika asubuhi hii Mikocheni jijini Dar es salaam.
 Wageni mbalimbali wakipata kifungua kinywa katika hafla hiyo.
 Wageni waalikwa katika uzinduzi huo wakibadilishana mawazo.
 Watoto kutoka shule ya msingi ya Ushindi Mikocheni wakiimba wimbo wa taifa katika hafla hiyo.
 Mjumbe wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Zuhura Sinare Murro, katikati ni Mgoyela.
Mjumbe wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Zuhura Sinare Murro akionyesha ngua zilizopo katika duka hilo.
 Wageni waalikwa wakiangalia nguo katika duka hilo.
Mdau Fredrick  Njoka  akiangalia suti katika duka hilo.
Habari na matukio na Full Shangwe

No comments:

Post a Comment