NJOMBE

NJOMBE

clock

Friday, March 16, 2012

Onyo kwa wapenzi wa 'Chumvini'


Jamani, leo naongelea mambo nyeti. Kwa hiyo nyie watoto wadogo...ONDOKENI!


Kuna huo mchezo katika ngono wa kumfurahisha mpenzi kwa kunyonya huko sehemu za siri. Sasa wataalamu wanasema kuwa mwanaume anaweza kuambukizwa HPV, yaani virusi vinavyosababisha ugonjwa wa kansa ya kizazi.


Mungu atunusuru, kwanza tunaambiwa kuwa wanaume wanaweza kuambukiza wanawake hiyo HPV na kusababisha kansa ya kizazi. Sasa wanaume nao wanaweza kuambukizwa na kupata kansa ya koo na mdomo! Duh!


Licha ya HPV kuna HIV unaosababisha ugonjwa wa UKIMWI. Nadhani mwisho watu wataishia kujifurahisha wenyewe maana magonjwa yamezidi! Kila siku kuna kipya!


Nawashauri kila mwaka mfanye physical check-up. Kwa wanawake in maana mfanye Pap Smear, hapo watajua kama una HPV au la. Daktari anakata kipande cha mlango wa kizazi (cerivx) na kuipima. Uzuri unatibika ukikamatwa mapema.

No comments:

Post a Comment