NJOMBE

NJOMBE

Friday, March 16, 2012

Kila siku unakimbiwa na wanawake, umegundua sababu?

NI kawaida yangu siku kama ya leo kukutana nanyi katika ukurasa huu wa kuzungumzia mapenzi. Nasema karibuni sana marafiki zangu tupate darasa maridhawa la kudumisha uhusiano wetu na wapenzi wetu.
Let’s Talk About Love ni kwa ajili ya marafiki wote. Wanaume kwa wanawake, ila kiukweli mada nyingi huegemea zaidi kwa wanawake. Hii inatokana na ukweli kwamba wao ndiyo walengwa hasa wa matatizo katika mapenzi. Huu ndiyo ukweli, ila leo nitazungumza zaidi na wanaume wenzangu.

Wewe mwanaume unayesoma hapa, jiulize; huwa unadumu na mwenzi wako? Unaachwa au kukimbiwa baada ya muda mfupi? Kama jibu ni ndiyo, hapa utapata tiba. Sikia nikuambie, wapo wengi ambao kila wakianzisha uhusiano, siku mbili tatu, mwanamke anamkimbia.
Anampenda sana, anamfanyia kila kitu ambacho yeye anaamini kinakidhi kwa mwanamke wake, lakini baada ya muda mfupi sana, anaachwa! Anabaki kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Rafiki yangu, lazima ujue kwamba pamoja na kuwa mapenzi hayana kanuni za moja kwa moja, zipo ndogo ndogo ambazo zikifuatwa, mateso kwako yatakuwa ni kitendawili.
Huwezi kukimbiwa na wanawake bila sababu za msingi, lazima kuna kitu kinachosababisha uachwe. Hapo sasa hakuna sababu moja, wewe ukiachwa kwa sababu hii, mwingine atakimbiwa kwa sababu ile. Katika darasa hili, ukijifunza kwa umakini utaweza kujua kasoro yako ilipokuwa na kufanya mabadiliko ili ‘usiachike’ tena!
Wanaume huwa wanawalaumu zaidi wanawake kutokana na sababu za hapa na pale zinazosababisha kuachana kwao. Lakini wengine hutoswa bila kuelezwa sababu za msingi, akibaki na maswali mengi lakini mwisho hupata msichana mwingine kabla ya kuachana naye tena bila kujua sababu halisi.
Wakati mwingine sababu zenyewe huwa za maana lakini zingine mh! Ni aibu kuzitaja hadharani. Hata hivyo, kuna wengine huamua kuachana na wapenzi wao kwa makosa ambayo wao hudhani ni makosa kumbe wao ndiyo wanaokosea! Hebu tuone…

UKOJE?
Kama una tatizo la kuachana na wapenzi kila wakati, kipegele hiki kinakuhusu! Anza kuangalia tabia zako upya. Unaishije na mpenzi wako, jirani zako na watu wanaokuzunguka? Unatumiaje ulimi wako? Wasichana wengi wanapenda wanaume wachangamfu na wacheshi wakiamini kwa namna moja ama nyingine, ni burudani kwao lakini huwa hawapendi kabisa uwachangamkie wengine kupita kiasi.
Wanaume wengi hupingana na hili lakini utafiti unaonyesha kwamba, asilimia 70 ya wanaume wanaowachangamkia sana wanawake, mwisho wake hufanya nao mapenzi kama siyo kuingia katika uhusiano moja kwa moja. Usibishe, tafiti uone!
Kama una tabia hii, hata kama unaamini kwamba uchangamfu wako siyo wa nia mbaya kwa wanawake, achana nao maana unamkwaza mpenzi wako bila kujua. Wakati mwingine anaweza kuonyesha wivu lakini mwingine hawezi kusema, hivyo hubaki akiumia moyoni mwake lakini akichoka huamua kuachana na wewe hata kama anakupenda akihofia kuwa katika penzi la kuchangia. Angalia vizuri tabia zako katika kipengele hiki.

MWANAMKE MATUNZO!
Hapa jamani inabidi tuambiane ukweli, tena bila kufichana! Kuna baadhi ya wanaume ni wabahili sana, yaani kutoa fedha kwa wapenzi wao wanaona shida sana. Visingizio vya kwamba wao siyo mabuzi ndiyo vimewajaa akilini mwao.
Utawasikia wakisema; “Mimi siyo buzi bwana, demu wangu halafu nimlipie? Haiwezekani!” Achana na hizo fikra ndugu yangu. Unatakiwa utoe matunzo kwa mpenzi wako. Siyo lazima mpaka akuambie! Ni jukumu lako kufahamu aina za vipodozi anavyotumia.
Mnunulie bila kukuambia, mpelekee, kuwa mbunifu, ukiona nywele zake zinaanza kufumuka, mpe fedha ya saluni, tena ikiwezekana mchagulie mtindo uupendao. Leo asuke rasta za kimasai, baada ya wiki kadhaa unambadilishia mtindo mwingine.
Jiulize kama wewe ndiye mpenzi wake halafu unakataa kumpa matunzo, unataka nani amhudumie? Hivi ulivyokutana naye akiwa mzuri, anapendeza unadhani ni nani aliyekuwa anamhudumia?
Nakuhakikishia ndugu yangu, kama huna utamaduni wa kutoa matunzo kwa mpenzi wako tarajia kukimbiwa! Kwa maneno mengine ni kwamba, kama hutoi matunzo kwa mpenzi wako ni kama umemruhusu awe katika uhusiano na mwanaume mwingine ambaye atatoa matunzo.
Ni wajibu wako kumnunulia mavazi, manukato na hata fedha za matumizi yake binafsi. Tatizo hili huwakumba hata wanandoa, hawataki kuwahudumia wake zao, wakidai kwamba wameshaoa! Usimpompendezesha atapendeza? Na asipovutia unadhani nini kitafuata kama siyo kutafuta mwanaume mwingine nje? Upo tayari kusalitiwa?

No comments:

Post a Comment