NJOMBE

NJOMBE

Saturday, March 31, 2012

HAFLA YA KUTOA TUZO ZA (EJAT) KWA WANAHABARI YAFANYIKA USIKU WA 30 MARCH DIAMOND JUBILEE

  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo kunafanyika hafla kubwa ya utoaji wa tuzo ya Umahili wa uandishi wa habari kwa mwaka wa 2012 zinazoandaliwa na Baraza la Habari MCT na washirika wake ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Jakaya Kikwete.
Wamejitokeza wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wasomi na waandishi wa habari wakongwe kama picha ya kwanza inavyoonekana kutoka kulia ni Profesa Aisha Yahya Othman mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mlimani, Jenrrali Ulimwengu, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliyesimama na Profesa Shivji kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika hafla hiyo usiku huu.
 Hawa ni miongoni mwa majaji kulia ni Itillio Tagalile, Afisa Uhusiano wa Tanesco Badra Masoud na Wenceslaus Mushi wakijadili jambo.
 Kushoto ni Awaichi Mawala kutoka Zantel na Mkurugenzi Msaidizi wa CCBRT Haika Mawala
 Wageni waalikwa kutoka mashirika mbalimbali nao wamehudhuria katika hafla hiyo.
 Majaji wakiwa katika meza yao.
 Mwenyekiti wa bodi ya TANAPA Modestus Lilungulu  kushoto na mjiumbe wa bodi Dk.Marcelina Chijoriga kulia wakiwa katika hafla hiyo.
 Waziri wa habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Katibu mtendaji wa Baraza la Habari MCT Kajubi Mukajanga.
 Mhariri kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo Jaquiline Liana akizungumza na Mkurugenzi wa Gazeti la Jambo Leo Juma Pinto kulia.
 Clement Mshana Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji TBC akizungumza na Profesa Helmasi Mwansoko Mkurugenzi wa Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
 Wadau kutoka Shelutete kutoka TANAPA na Geofrey Tengeneza kutoka TTB nao wapo katika hafla hiyo.

 Wanaharakati kutoka taasisi mbalimbali nao wamejongea katika hafla hiyo.
 Kutoka kulia ni Mbunge wa Kondoa Kusini akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya bia ya Serengeti Graham Anderws
 Bendi ya Msondo ikitumnuiza katika hafla hiyo.
Mzee wa Kammbi popote Antonio Lugas akiwa na mdau Abel Onesmo kutoka Clouds FM

No comments:

Post a Comment