NJOMBE

NJOMBE

Wednesday, September 18, 2013

MUME ANASA PICHA ZA UCHI ZA MKEWE AKIWA NA MWANAUME MWINGINE

                  Mke wa mtu, Rehema Mboje akiwa amelala gesti.

Mwanaume mfanyabiashara wa jijini Dar aitwaye Joseph Mboje, amenasa picha za mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Rehema akimtuhumu kusaliti ndoa yao na mwanaume mwingine. 
Mboje alidai kuwa kwa muda mrefu alikuwa akimhisi mkewe ‘kucheza nje kapu’ na mwanaume mwingine ambapo katika pekuapekua yake ndipo akanasa picha hizo kwenye simu yake kabla ya hivi karibuni kutengana kabisa.

  
Kwa mujibu wa Mboje, baada ya kumgundua na kunasa matukio yake na mwanaume nje ya ndoa hasa gesti, mkewe huyo aliondoka nyumbani maeneo ya Manzese, Mtaa wa Sisi-Kwasisi, Dar, bila kujua alikohamia lakini alipofanya uchunguzi akabaini ana mwanaume mwingine.


“Sikuacha kupeleleza, nikaambiwa na mtu wangu wa karibu kuwa chanzo cha mke wangu kuondoka nyumbani ni kijana mmoja tuliyewahi kumwajiri katika biashara zetu,” alisema Mboje.
 Rehema Mboje akiwa na mwanaume mwingine
  Huku akizungumza kwa uchungu, jamaa huyo alisema kuwa kijana huyo aliletwa na mkewe kama meneja wa baa yao iliyopo Kinondoni-Mkwajuni, Dar lakini baada ya muda aliona mabadiliko makubwa kutoka kwa mkewe, jambo lililomshtua kwani alianza kuwa mlevi wa kupindukia na kurudi nyumbani usiku wa manane.


Alidai kuwa baada ya kushtuka, alimuuliza mkewe huyo kuhusiana na hali hiyo ya kuvuka kiwango hadi kujifotoa akiwa na mwanaume nje ya ndoa lakini alikana.
  
Mboje alidai kuwa aliendelea kufuatilia nyendo zao kwa kipindi cha miaka mitano, mwaka wa sita ambao ndiyo huu, mambo yakawa wazi kuwa mkewe wa ndoa aliyedumu naye kwa miaka 17, anatembea na kijana huyo aliyemtaja kwa jina moja la Lwalwai.
  
“Nimeumia sana, sikutarajia kama mke wangu anaweza kunifanyia hivi,” alisema.


Rehema alipotafutwa  alianza kwa kumkandia mumewe na kusema hamtaki tena.
  
Alipobanwa na wanahabari wetu, alikiri kuwa Mboje alikuwa mumewe na kwamba amezaa naye watoto wawili na kuishi pamoja kwa miaka 17 kabla ya ndoa kuvunjika.

Alisema kwa sasa maisha aliyoamua kuishi anayajua mwenyewe hivyo kila mtu achukue hamsini zake.
  
Mwanamke huyo pia alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Lwalwai tangu kipindi cha nyuma na hii yote alifanya kutokana na tabia za mumewe ambazo hakutaka kuziweka wazi.
  
Alisema kwa sasa anaishi peke yake na kama huyo mumewe ataanza kumfuatafuata huenda akaamua kuolewa na Lwalwai.
  
Kwa upande wake, Lwalwai alisema kuwa ni kweli alikuwa na uhusiano na Rehema lakini hakujua kama ni mke wa mtu ndiyo maana alikubali kushirikiana naye kimapenzi pamoja na kuwa alikuwa anafanya kazi kwake.

No comments:

Post a Comment