Kiongozi wa chama cha New
Democracy nchini Ugiriki, chenye sera za mrengo wa kulia, Antonis
Samaras, ameshinda katika uchaguzi mkuu wa pili ambao umefanyika wiki
sita baada ya ule wa kwanza.
Bwana Samaras amesema wananchi wa Ugiriki
wameeleza nia yao ya kutaka kubakia katika muungano wa nchi za Ulaya na
kuheshimu nia ya nchi hiyo katika kuimarisha uchumi wake.Bwana Tsipras amesema chama chake bado kinapinga hatua zilizopendekezwa na nchi wanachama wa Euro kuimarisha uchumi wa Ugiriki.
Akiwahutubia wafuasi wake mjini Athens, Bwana Tsipras amesema kukiunga mkono chama cha Syriza kumezionyesha nchi za Ulaya na viongozi wa siasa wa Ugiriki kwamba hawawezi kuweka masharti ya kunusuru uchumi wa nchi hiyo bila kukubaliwa na wananchi.
Viongozi wa nchi za Ulaya walionya kuwa ikiwa raia wa Ugiriki watapinga mpango huo uliopendekezwa wa kufufua uchumi wao, basi nchi hiyo italazimika kuacha kutumia sarafu ya Euro.
Waziri wa Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble amesema matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha nia ya raia wa nchi hiyo kuendelea na mpango wakunusuru uchumi wa nchi yao.
Mawaziri wa fedha kutoka nchi wanachama wa umoja wa ulaya, katika taarifa ya pamoja wameelezea kuwa wawakilishi wa benki kuu ya umoja huo, shirika la fedha duniani (IMF) na tume ya umoja huo watazuru nchi hiyo punde tu serikali mpya itakapoundwa.
No comments:
Post a Comment