NJOMBE

NJOMBE

Friday, July 6, 2012

Kenya haitanunua mafuta tena Iran


Kiwanda cha mafuta Iran
Kenya imefutilia mbali mipango ya kununua mafuta ghafi kutoka nchini Iran, baada ya kutishiwa kuwekewa vikwazo. Hii ni kwa mujibu wa afisaa mkuu katika wizara ya kawi ya Kenya.
Kulingana na mkataba uliokuwa umefikiwa kati ya Kenya na Iran mwezi jana , nchi hiyo ilinuia kununua tani milioni nne za mafuta kutoka kwa kampuni ya kitaifa ya mafuta ya Iran.
Lakini ubalozi wa Marekani nchini Kenya ulionya kuwa ni muhimu kusitisha mpango wowote utakaoipa mapato zaidi serikali ya Iran.
Marekani kwa ushirikiano na muungano wa ulaya wameweka vikwazo zaidi dhidi ya Iran kufuatia wasiwasi kuhusu mpango wake wa nuclear.
"Kwa sababu ya shinikizo za kimataifa , tumelazimika kusitisha mpango wetu" alinukuliwa akisema katibu katika wizara ya kawi nchini humo, Patrick Nyoike.
Mnamo siku ya jumapili, Muungano wa Ulaya uliwekea Iran vikwazo kamili vya kuuza nje mafuta, kuambatana na sheria ya Marekani ambayo inawekea vikwazo mshirika yeyote anayejihusisha na benki kuu ya Iran.
"Kuna vikwazo sasa dhidi watu watakaonunua mafuta na bidhaa zingine za mafuta kutoka kwa Iran, watachukuliwa hatua" alisema balozi anayeondoka wa Marekani nchini Kenya Scott Gration mnamo Jumatano kuhusu mipango ya Kenya kununua mafuta kutoka Iran.
Mwezi jana, maafisa katika mtambo wa pekee wa kusafisha mafuta nchini Kenya, walisema kuwa wataanza kununua mafuta ghafi.

No comments:

Post a Comment