NJOMBE

NJOMBE

Sunday, September 2, 2012

Dos Santos aelekea kushinda

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Angola yanaonesha kuwa chama tawala cha MPLA kimepata robo tatu za kura - zimepungua kidogo kushinda uchaguzi uliopita.
Rais dos Santos wa Angola baada ya kupiga kura
Endapo idadi hiyo itathibitishwa matokeo yake ni kuwa Rais Jose Eduardo dos Santos, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30, atapata muhula mwengine wa uongozi.
Uchaguzi huo, wa tatu tangu Angola kupata uhuru mwaka wa 1975, ulikwenda vema ingawa awali kulikuwa na taarifa za ulalamishi.
Zamani Angola ilivurugwa na vita lakini katika miaka ya karibuni imepata utajiri wa mafuta.

No comments:

Post a Comment