NJOMBE

NJOMBE

Sunday, September 2, 2012

Kituo cha televisheni Misri chafungwa


Tajiri anayemiliki kituo cha televisheni nchini Misri amefikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kusema kuwa Rais Mohamed Morsi afaa kuuwawa.
Mji wa Cairo kwenye kituo cha televisheni cha Al-Faraeen
Tawfiq Okasha alikanusha kuwa amefanya uchochezi, na kusema kuwa alilalamika tu juu ya Rais Morsi.
Alisema kesi hiyo ni ya kisiasa, na kusema kuwa Muslim Brotherhood - chama cha Rais Morsi - kinataka kunyamazisha malalamiko.
Kituo cha televisheni cha Bwana Okasha, Al-Faraeen, kilifungwa kwa muda awali mwezi uliopita.
Kimetangaza maoni makali dhidi ya chama cha Brotherhood.

No comments:

Post a Comment