NJOMBE

NJOMBE

clock

Tuesday, September 11, 2012

Ethiopia kuwaachilia wandishi wa kigeni


Martin Schibbye na Johan Persson
Ethiopia imewasamehe waandishi habari wawili raia wa Sweden waliofungwa jela nchini humo mwaka jana kwa madai ya kuunga mkono vitendo vya kigaidi.
Wawili hao wanatarajiwa kuachiliwa baadaye wiki hii
Martin Schibbye na Johan Persson walikuwa wanahudumia kifungo cha miaka 11 baada ya kukamatwa mwaka jana mwezi wa saba na waasi mashariki mwa Ethiopia.
Duru za serikali zilisema kuwa waandishi hao walisamehewa na hayati Meles Zenawi kabla ya kifo chake mwezi jana.
Wamekuwa wakidai kuwa walikuwa tu nchini Ethiopia kikazi.
Schibbye na Persson, waliomba kuachiliwa baada ya hukumu yao mwaka jana kwa madai ya kuunga mkono kundi la wapiganaji la Ogaden (National Liberation Front (ONLF), ambalo Ethiopia inawaona kama kundi la kigaidi.
Afisaa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kujulikana, alisema kuwa waandishi hao wataachiliwa wiki hii pamoja na wafungwa wengine 1,900.
Mwaka mpya wa Ethiopia ambapo wafungwa huachiliwa, utasherehekewa siku ya Jumanne.
Meles,ambaye alikuwa mamlakani kwa miaka 21 alifariki mwezi jana baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Serikali imesema kuwa naibu wake Hailemariam Desalegn, ataapishwa kuhudumu hadi uchaguzi mpya utakapofanyika mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment