NJOMBE

NJOMBE

Friday, September 14, 2012

Washukiwa wa mashambulizi wakamatwa Libya


Kundi linaloshukiwa kuafnya mashambulizi mjini Benghazi
Maafisa nchini Libya wamewakamata washukiwa kadhaa wa machafuko yaliyosababisha kifo cha balozi wa Marekani nchini humo pamoja maafisa wengine wanne wa ubalozi huo mjini Benghazi.
Waziri mkuu mpya wa Libya Mustafa Abu Shaqur aliambia BBC kuwa uchunguzi unaoendelea kuhusiana na kisa hicho unaonekana kufanikiwa.
Shambulizi lilifanyika siku ya Jumanne wakati wa maandamano yaliyopinga filamu iliyotengezwa nchini Marekani kumkejeli Mtume Mohammed.
Maandamano sawa na hayo yamesambaa katika nchi za kiarabu na mataifa ya Kaskazini mwa Afrika.
Maandamano zaidi yanatarajiwa kufanyika baada ya maombi ya Ijumaa
Makabiliano kati ya polisi wa kupambana na ghasia pamoja na waandamanaji yameendelea usiku kucha katika mji mkuu wa Misri, Cairo ambako makundi ya wapiganaji wa kiisilamu pamoja na watu wengine waliitisha maandamano ya amani ya watu milioni moja baadaye leo Ijumaa.
Hapo jana kulizuka ghasia zaidi nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kati ya polisi na waandamanaji wanaokashifu filamu ambayo wanasema kuwa inakejeli imani ya Kiislamu.
Runinga ya Misri ilionyesha gari likiteketezwa moto na watu wengine wakikimbia vitoza machozi.
Waandamanaji walitaka kufukuzwa kwa balozi wa Marekani nchini humo huku polisi wakiwafyatulia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.
Nchini Yemen waandamanaji walivamia ubalozi wa Marekani wakichoma moto magari kabla ya vikosi vya ulinzi kuwadhibiti kwa kuwafukuza kutoka eneo hilo.
Maandamano zaidi pia yamefanyika katika nchi za Tunisia, Morocco, Sudan, Mauritania na Iran.
Wakati huohuo maafisa wa Marekani wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni ya kupangwa au la .
Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .
Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba makundi ya jihad huenda yalihusika .
Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume Mohammed.
Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .
Aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya Christopher Stevens
Awali waandamanaji walirusha mawe kwenye ubalozi huo na vikosi vya usalama vikafyatua mabomu ya kutoa machozi kuwa tawanya.
Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika

No comments:

Post a Comment