NJOMBE

NJOMBE

clock

Tuesday, September 4, 2012

Zenawi kujengewa kaburi la makumbusho

 
Marehemu Meles Zenawi
Ethiopia imetangaza itajenga kaburi la makumbusho ili kuenzi maisha ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Marehemu Meles Zenawi aliyezikwa jumapili iliyopita.
Kaimu Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn amesema kaburi hilo la makumbusho litajumuisha maktaba na maonyesho ya maisha ya Meles Zenawi pamoja na mafanikio yake.
Maelfu ya raia wa Ethiopia wakiwemo viongozi maarufu pamoja na viongozi wa nchi mbali mbali walihudhuria mazishi ya kiongozi huyo yaliyofanyika hapo jana.
Marehemu Zenawi alifariki mwezi uliopita Brussels baada ya kuwa madarakani kwa miaka 21.
Hadi sasa sababu za kifo cha kiongozi huyo aliyefariki akiwa na miaka 57 bado hazijajulikana.
Marehemu Zenawi amekuwa akisifiwa kwa kuleta maendeleo nchini mwake baada ya nchi hiyo kupitia katika vipindi virefu vya ukame na njaa.
Hata hivyo amekuwa akikosolewa kwa kukandamiza upinzani na mashirika ya kijamii pamoja na uhuru wa waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment