NJOMBE

NJOMBE

Friday, August 24, 2012

Breivik siyo mwendawazimu

Mahakama ya Norway yameamua kuwa Anders Behring Breivik ana akili zake timamu, na imemhukumu kifungo cha miaka 21 kwa kuuwa watu 77 mwezi wa Julai mwaka jana.
Breivik anatabasamu
Upande wa mashtaka ukitaka kupata uamuzi juu ya akili ya Breivik, na angekutikana punguani angewekwa kwenye jela ya wendawazimu kwa muda usiojulikana.
Breivik siku zote amekiri kufanya mashambulio ya mabomu na bunduki, bila ya kuonesha majuto.
Amekuwa akishikilia kuwa ana akili yake, na kwamba aliyofanya ni vitendo vya kisiasa.
Alitabasamu hukumu ilipotolewa.
Wakili wa Breivik amethibitisha kuwa mteja wake hataomba rufaa.

No comments:

Post a Comment