NJOMBE

NJOMBE

Tuesday, August 21, 2012

Kazi yakoma mgodi wa Lonmin


Wafanyikazi wa Lonmin
Wachimba migodi waliofika kazini lakini pasipo kufanya kazi
Wafanyikazi wa migodi nchini Afrika Kusini wameanza kurudi mmoja mmoja katika migodi ya dhahabu nyeupe, platinum, ambako polisi waliwafyatulia risasi wenzao na kusababisha vifo vya watu 34 Alhamisi iliyopita.
Hata hivyo idadi ya wachimba migodi hao haijatosha kiasi cha shughuli za uchimbaji migodi kuendelea kikamilifu.
Kampuni ya Lonmin ilitangaza kwamba imeanza tena shughuli zake, lakini ukweli ni kwamba ni chini ya theluthi moja tu ya wafanyakazi waliofika katika migodi, na kazi haijaanza.
Kampuni pia ilitangaza kwamba imetenga muda wa wafanyakazi wote kurudi kazini, na kuongezea muda huo hadi Jumanne.
Imetisha kwamba watakaoshindwa kufanya hivyo, basi watafutwa kazi.
Rais Jacob Zuma alitangaza wiki nzima ya maombolezi kufuatia vifo hivyo vya wachimba migodi.
Vile vile alitaka uchunguzi kamili kufanyika.

No comments:

Post a Comment