NJOMBE

NJOMBE

Thursday, August 16, 2012

Rais wa Nigeria ataka mabadiliko

Rais Goodluck Jonathan
Rais Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, ameamuru mabadiliko yafanyike katika sekta ya michezo baada ya taifa hilo kukosa kushinda hata medali moja katika michezo ya Olimpiki.
Waziri wa Habari Labaran Maku amesema rais anataka mageuzi makubwa katika sekta hiyo ili kurejesha hadhi ya taifa hilo katika michezo.
Wachanganuzi wanasema, matokeo ya Nigeria katika mashindano ya olimpiki ya London mwaka huu yalikuwa mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Rais Jonathan, aliwasilisha suala hilo wakati wa kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika katika mji mkuu Abuja.
''Naamini kile taifa hili linahitaji kwa sasa ni kutathmini kile kilichotendeka na kufanya mabadiliko, ili kurejesha heshima na hadhi ya taifa hilo'' alisema Bwana Maku.
Nigeria ndilo taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika, na linajihisi kama taifa lenye ushawishi mkubwa zaidi.
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton, amesema hatma ya Nigeria siku zijazo ni nzuri ikiwa taifa hilo litaendeleza mikakati yake ya kupambana na ufisadi.
Bi. Clinton aliyasaema hayo wakati alipofanya kikao na rais Goodluck Jonathan, katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja.
Nigeria ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta duniani, lakini viwango vya ufisadi viko juu zaidi, hali ambayo imehujumu ufanisi wa taifa hilo.

No comments:

Post a Comment