NJOMBE

NJOMBE

Sunday, August 26, 2012

Gambia yaanza tena kunyonga wafungwa

Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinaadamu, Amnesty International, linasema limeambiwa kwamba Gambia imewanyonga wafungwa tisa kati ya 47 ambao wamehukumiwa kifo.
Rais wa Gambia, Yahya Jamme
Msemaji wa Amnesty, Lisa Sherman Nichols, aliiambia BBC kwamba wafungwa hao ni wa mwanzo kunyongwa nchini Gambia kwa miaka 29, na inasemekana alikuwako mwanamke kati yao, na wananchi watatu wa Senegal.
"Tumepata taarifa za kuaminika kuwa watu 9 walinyongwa jana usiku.
Nimezungumza na baadhi ya jamaa zao, ambao bila ya shaka wako kwenye majonzi, na wametuomba tuchukue hatua.
Wamegusia kuwa kuna wengine watanyongwa leo usiku.
Tunajaribu kuzitawanya habari hizi ulimwenguni na serikali ya Gambia inafaa kujua kuwa macho ya ulimwengu na serikali za nchi za nje yameelekezwa juu ya nchi hiyo."
Hapo awali, shirika la raia la nchi hiyo lilimlaumu rais wa Gambia, Yahya Jammeh, na lilisema kwamba wengi waliohukumiwa kifo ni wafungwa wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment