NJOMBE

NJOMBE

Saturday, August 25, 2012

Risasi zafyatuliwa katikati ya New York

Watu kadha wamepigwa risasi nje ya jengo maarufu la skyscraper mjini New York, Empire State Building, ambalo linavutia watalii.
Empire State Building mjini New York
Meya wa New York, Michael Blomberg, alisema baadhi ya wale waliojeruhiwa pengine walipigwa risasi za polisi, lakini alisema majeruhi siyo mahtuti.
Mshambuliaji huyo ametajwa kuwa John Jeffrey Johnson - mpambi wa maduka ya nguo, ambaye alitolewa kazini mwaka jana.
Mtu aliyemuuwa ni mfanyakazi mwenzake wa zamani.
Eneo hilo la misafara mingi ya magari katika mtaa wa Manhattan, limefungwa na magari hayaruhusiwi kupita.

No comments:

Post a Comment