NJOMBE

NJOMBE

Friday, August 24, 2012

Uingereza yaibembeleza Ecuador

Uingereza imeandika barua kwa ubalozi wa Ecuador mjini London ikitaka kurejelea mazungumzo kuhusu hatma ya Julian Assange, mwanzilishi wa mtandao wa kufichua siri wa Wikileaks, aliyetorokea katika majengo ya ubalozi huo kuepuka kurejeshwa nchini Sweden kwa lazima.
Julian Assange katika ubalozi wa Ecuador
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulivurugika baada ya uamuzi wa Ecuador kumpa bwana Assange hifadhi ya kisiasa na Uingereza kutishia kuvamia ubalozi huo na kumkamata.
Afisi inayoshughulika na masuala ya kigeni haijasema chochote kuhusu ujumbe uliokop kwenye barua hiyo lakini afisa mmoja ameelezea kuwa inanuia kutuliza hali kati ya mataifa hayo mawili.
Rais Rafael Correa ameiambia BBC kuwa Uingereza ilifanya makosa makubwa kwa kutishia kuingia kwa nguvu kwenye ubalozi wa Equador,''Huu ni mvutano ambao ungeisha iwapo Uingereza ingetoa hakikisho ya kupita kwa usalama kwa Bwana Assange au unaweza kuendelea kwa miezi na hata miaka iwapo hataweza kutoka kwenye ubalozi wetu hapa London kuelekea Equador.''
Huenda mataifa ya Amerika Kusini yakamuunga mkono rais Rafael Correa.
Huku Uingereza ikisema kuwa inataka kurejelea mashauriano kuhusu hatma ya Julian Assange, Equador haikubaliani na msimamo huo na inataka kuhakikishiwa kuwa Assange hatakamatwa iwapo atatolewa kwenye ubalozi wao nchini Uingereza kuelekea Equador.
Equador inataka pia kuhakikishiwa kuwa mwanzilishi huyo wa mtandao wa Wiki Leaks hatawahi kupelekwa Marekani anakokabiliwa na tuhuma za kutoa taarifa muhimu na za siri kwenye mtandao wake.
Hata hivyo hakuna matumaini kwamba Marekani itakubali hilo.
Kwa hiyo ubalozi wa Equador umekiri kuwa huenda ukampa bwana Assange hifadhi kwa miaka mingi.

No comments:

Post a Comment