NJOMBE

NJOMBE

Sunday, August 26, 2012

Mwana anga mkongwe wa Marekani afariki

Rais Obama ameongoza katika sifa na rambi-rambi zilizotolewa baada ya kifo cha Neil Armstrong, mwana anga wa kwanza kutua kwenye mwezi, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 82 kutokana na matatizo aliyopata baada ya upasuaji aliofanyiwa kwenye moyo.
Neil Armstrong
Mwenzake Armstrong katika safari ya kihistoria ya kwenda mwezini mwaka wa 1969 alikuwa Buzz Aldrin, ambaye alisema Armstrong alikuwa rubani na kamanda mahiri.
Familia ya Neil Armstrong imetoa wito kwa Wamarekani kuonesha heshima zao kwa kufuata mfano wake wa kutumika, kufanikiwa na bila ya majivuno.
Taarifa ya familia iliwaambia wale washabiki wake: "ukitembea nje usiku ukaona mwezi unakuchekea, mfikirie Neil na umkonyeze."

No comments:

Post a Comment