WANANCHI wa Mtama wilayani Lindi mkoani humo wametaka Katiba mpya kuwa na
kipengele cha kuhakikisha rasilimali za nchi zinamilikiwa na Serikali, ili
kuondoa ukoloni mambo leo uliopo sasa.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari
Namupa, Kaspal Mtotomwema, alisema hayo jana wakati
alipokuwa akizungumza
kwenye mdahalo ulioandaliwa na Mtandao Lingonet.
Alisema ikiwa
rasilimali zitamilikiwa na Serikali, itasaidia wananchi kumiliki ipasavyo
rasilimali hizo kuliko ilivyo sasa ambapo watu wachache wanamiliki maeneo ya
ardhi, migodi na kusababisha jamii kuwa watumwa ndani ya nchi yao.
Alitoa mfano kuwa hivi sasa kuna mfumo wa soko huria ambao wale wenye
uwezo watakuwa
nanafasi nzuri ya kufanya kila kitu na jamii wenye kipato cha
chini watabakia kunyonywa ndani ya nchi yao daima.
Mtotomwema alisema
watu wachache wanamiliki migodi, ardhi na viwanda kutokana kufuatwa
mfumo
huo ni hatari kiuchumi katika nchi.
Aliongeza nchi haiwezi kuwa na
maendeleo ikiwa haina vyanzo vya mapato na kubakia kutegemea wahisani au kundi
la matajiri wanaomiliki uchumi wa nchi.
Mkazi wa Kijiji cha Mtama,
Dustan Millanzi alitaka Katiba liwe somo lianzie elimu ya msingi
na
kuendelea.
Alisema yeye ana umri wa miaka 30, lakini katiba aliiona kwa
macho jana na miaka yote hiyo 29 alikuwa haifahamu wala umuhimu wake, kwa
biandamu.
Naye Mwanasheria Khalfan Omary aliwataka wananachi kuanza
kujadili na kuilewa Katiba
na kuhakikisha wanatoa michango yao wakati Tume
ya Kukusanya Maoni ikifika kwao.
Alisema Katiba ni muhimu kwa maisha ya
Mtanzania kwa kuwa inamgusa kwenye vipengele
vya kiuchumi, utawala na
siasa.
No comments:
Post a Comment