WANANCHI wa Kijiji cha Mbebe Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya wamelazimika kutoka na
taa zao nyumbani mpaka Kituo cha Afya cha kijiji hicho ili kupatiwa huduma baada
ya kituo hicho kukosa umeme kwa muda mrefu.
Watumishi wa kituo hicho
waliojitambulisha kwa jina moja moja la Pagale na Kaponda walisema tatizo la
umeme limekuwa kero hasa kwa wanawake wajawazito wanaojifungua usiku.
Wahudumu hao walisema wagonjwa wanaopatiwa huduma katika kituo hicho ni
kutoka vijiji saba vinavyoizunguka zahanati hiyo na wengi wao wakiwa wanatoka
umbali wa kilometa saba na wengine tano.
Aidha, walisema tatizo hilo
linawalazimu mara nyingine kutumia mafuta yao ya taa huku nishati hiyo ikiwa
imepanda bei kwa kiasi kikubwa na hivyo kuwa kero kwao.
Kwa Shirika la
Biashara la Taifa (ZSTC), baadhi ya wananchi walihoji pesa wanazotoa katika
kituo hicho kuwa zinafanya kazi gani mpaka kituo hicho kinakosa umeme.
“Hapo nyuma umeme ulikuwepo lakini kutokana na wananchi kusuasua kulipia
bili za umeme, umeme ukakatwa,” alisema mmoja wa wauguzi ambaye hakutaka jina
lake liandikwe gazetini.
Aidha alisema kitendo hicho kimewasababishia
wachukiwe na wananchi kwa kuwa wagonjwa wafikapo kituoni hapo hukuta kukiwa giza
na ndugu wa mgonjwa hulazimika kutafuta mafuta ya taa.
Imeandikwa na Neema Kidumba, Mbeya;
No comments:
Post a Comment