KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini, imeitaka Wizara ya Nishati na Madini,
kuwasilisha mikataba ya kampuni za Mantra na Urinex, zinazojihusisha na
uchimbaji wa madini ya Uraniam, ili kuliwezesha Bunge kujiridhisha juu uhalali
wao katika kufanya shughuli hizo.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa
kamati hiyo, January Makamba, ambaye alisema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa
madini yenyewe katika dunia ya sasa.
Alisema kukaguliwa kwa mikabata
hiyo, kutasaidia kubaini uhalali na uwezo wa kampuni hizo katika kufanya
shughuli hizo.
“Kuna kampuni mbili za uchimbaji wa madini ya Uranium
hapa nchini, lakini hadi sasa mikabata yake hatujaiona, kwa hiyo tumeitaka
wizara kuwasilisha mikataba hiyo kwenye kikao kijacho cha Bunge ili tuweze
kuikagua,”alisema Makamba.
Alisema Kampuni ya Urinex inachimba madini
hayo katika maeneo ya Manyoni, mkoani Singida na Bahi huko Dodoma wakati Kampuni
ya Mantra, inachimba Uranium katika mikoa ya Kusini mwa
Tanzania.
Alisema Serikali kupitia kamati hiyo inapaswa kuhakikisha kuwa
madini yanawanufaisha wananchi kuiwezesha nchi kujiingizia
mapato.
Alisema madini hayo yanahitajika sana duniani katika shughuli
mbalimbali na kwamba kwa msingi huo kama lazima ijue mikabata yote inayohusu
uchimbaji wa Uranium.
Alisema kutowasilishwa kwa mikataba ya kampuni
hizo, kumeifanya kama yake, kushindwa kujadili suala lolote kuhusu kampuni
hizo.
No comments:
Post a Comment