MAJAMBAZI wanaosadikiwa kutoka nchi jirani ya Kenya wakiwa na silaha za moto na
mapanga wamevamia Kijiji cha Sirari na kumuua mkazi wa kijiji hicho ambaye ni
raia wa Kenya
aliyefahamika kwa jina la Babu Gimonge (25).
Mtu huyo
alikufa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali pajani.
Aidha kundi
lingine la watu wenye silaha lilivamia katika kijiji cha Kebeyo katika Tarafa ya
Inchungu na kufyatua risasi ovyo kabla ya kuingia kwenye nyumba za Magabe Robhi
Nyaibaru na Matiko Nyamhanga na kuwajeruhi kwa mapanga kabla ya kupora Sh
milioni 2.5.
Wakisimulia matukio hayo Mwenyekiti wa Mji Mdogo wa Sirari,
Nyangoko Paulo alisema tukio la kuvamiwa kwa Gimonge lilitokea saa 4 usiku
Jumatano Januari 12, mwaka huu.
Akimzungumzia Gimonge Mwenyekiti huyo
alisema nyumba yake ilikuwa umbali wa meta 400 kutoka mpaka wa Tanzania na
barabara ya Isebania nchini Kenya.
Katika tukio la pili, Diwani wa Kata
ya Mbogi Servester Nyankomo alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa
ambapo majambazi hao walifanya uhalifu huo kwa saa mbili katika kijiji hicho kwa
kuvamia nyumba za Magabe Robhi Nyaibaru aliyeporwa Sh milioni 2 na
nyumba ya
Matiko Nyamhanga aliyeporwa Sh laki tano na pia kuwajeruhi kwa mapanga.
Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Sirari, James Manyama amethibitisha kutokea
kwa matukio hayo na kusema Polisi inaendelea na msako wa watuhumiwa.
No comments:
Post a Comment