Niliondoka Singida Mjini saa kumi na moja alfajiri
kuelekea Dodoma. Kilomita 40 kutoka Manyoni nilikutana na hali hiyo pichani
kunako saa kumi na mbili na nusu. Eneo la tukio niliwakuta askari watano
wamevalia kiraia wakiwa na silaha za moto. Wameniambia tukio limetokea usiku wa
kuamkia leo majira ya kuanzia saa sita usiku na linawahusisha maja majambazi
wasiopungua wanane.
Kuna walioporwa fedha, simu na mali zao . Mahali hapa
kuna pori kubwa upande wa kushoto. Inaaminika majambazi hayo yenye silaha
yangali yamejiicha porini.
Hakuna aliyekamatwa. Nilishuhudia polisi hao wakifuatilia nyayo huku wakinionyesha mahali majambazi hayo yalilala chini kujificha wakisubiri giza na kuanza kupanga mawe yao. Kwa kusoma mazingira ya eneo kwangu mimi napata tafsiri kuwa majambazi hayo yalifanya maandzi ya mpango wao kwa siku kadhaa.

Maana, mawe hayo mazito yanaonekana kuwa yalikuwa
yakisogezwa usiku karibu na tukio na kufikia idadi waliyohitaji. Intelijensia ya
kipolisi ingefanya kazi yake sawa sawa na kwa kushirikiana na wenyeji
ingewezeza kubaini mapema movement ya mawe yale. Na katika dunia ya sasa , mbwa
wa polisi waliopewa mafunzo wangefanya kwa haraka na kwa ufanisi zoezi la
kufuatilia majambazi porini badala ya polisi kufuatilia nyayo kwa
macho.
No comments:
Post a Comment