SIKU chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji ( E W U R A )
kukubaliana na
Tanesco na kutangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia
40.29, sasa ni zamu ya Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco).
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji
zinasema gharama za maji zitapanda kunatokana na kupanda kwa gharama za umeme.
Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Jackson Midala, ametangaza kusudio hilo la
kupandishwa kwa gharama za huduma ya majisafi na majitaka.
Midala
alisema hayo juzi akiwa Bomu wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri
wa Maji, Gerson Lwenge, katika mtambo wa kusafisha na kusafirisha maji wa Ruvu
Chini alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari juzi.
Midala
alisema ongezeko hilo la bei litaongeza gharama za uzalishaji wa majisafi na
majitaka
na hivyo kuifanya Dawasco ilazimike kuwapandishia bei ya huduma ya
majisafi wateja wake.
Midala hakusema bei ya huduma hiyo itaongezeka kwa
kiasi gani, kutokana na Dawasco na
mamlaka zingine za majisafi na majitaka
nchini kutojipangia bei za huduma hiyo.
Aidha, Midala alieleza kuwa
mwishoni mwa mwaka jana, Dawasco ilipendekeza bei mpya za huduma ya majisafi na
kuwasilisha mapendekezo hayo Ewura. Hata hivyo Ewura hawakukubaliana na
mapendekezo hayo.
No comments:
Post a Comment