NJOMBE

NJOMBE

Thursday, July 5, 2012

Kuhesabu kura kurudiwa Mexico


Shughuli ya kuhesabu kura nchini Mexico
Shughuli ya kuhesabu kura nchini Mexico
Maafisa wa tume ya Uchaguzi nchini Mexico wameamuru shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi wa urais katika zaidi ya asilimia hamsini ya vituo kote nchini kurudiwa.
Hii ni baada ya makosa kupatikana wakati wa kujumuisha kura kutoka vituo hivyo.
Mgombea wa Urais anayeongoza, Enrique Pena Nieto, ameiambia BBC kuwa chama chake cha PRI, hakikununua kura wala kufanya makosa yoyote.
Wakati mgombea wa Urais, Lopez Obrador, alipowasilisha malalamishi yake kuhusu utaratibu wa uchaguzi huo wa Urais mapema wiki hii, hata wafuasi wake sugu hawakutarajia tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali kiasi hicho.
Maafisa hao wametoa amri kura kutoka vituo 143,000 kuhesabiwa tena.
Hatua hiyo inatarajiwa kuwaridhisha wafuasi wa Bw. Lopez, lakini itamsumbua mgombea anayeongoza, Enrique Pena Nieto.
Bw. Pena Nieto, amekuwa na matumaini ya kutangazwa rais wa Mexico katika muda wa siku chache baada ya uchaguzi wa Jumapili.
Hata hivyo madai kuwa chama chake kilinunua kura katika baadhi ya maeneo, yamesababisha kura kuhesabiwa upya.
Akizungumza na BBC Bw Pena Nieto amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa chama chake kilifuata utaratibu unaofaa.

No comments:

Post a Comment