NJOMBE

NJOMBE

Sunday, October 14, 2012

Mateso katika jeshi la Uturuki

Ripoti mpya kuhusu mateso ya wanajeshi wanaoandikishwa jeshini katika jeshi la taifa nchini Uturuki, imefichua kuwa mamia ya wanajeshi huteswa wakati wakihudumu jeshini.
Ripoti hiyo iliyochapishwa na shirika la kutetea haki za binadamu la (Rights of Conscripts Initiative), inasimulia visa vya waathiriwa mianne na thelathini na mbili wanaoelezea mateso waliyopitia.
Mmoja wa walioandika ripoti hiyo, alisema kuwa aliamini matokeo ya uchunguzi huo yalikuwa tu doa dogo kwani kuna mengi ya kushtua kuhusu visa vingi kama hivyo katika jeshi la Uturuki.
Zaidi ya vijana lakini nne huandikishwa jeshini kila mwaka nchini Uturuki.

No comments:

Post a Comment