Ni vigumu kuelezea moja kwa moja kujiamini
maana yake nini? Lakini mtazamo wa mwanadamu juu ya namna wenzake
wanavyomchukulia inaweza kuwa kutafsiri ya neno kujiamini. Ikiwa
utajilinganisha na wengine na hatimaye kuhisi aibu, ujue unakabiliwa na tatizo
la kujiamini.
Kimsingi kuna mambo mengi yanayoweza
kumfanya mtu asijiamini mbele ya wenzake, kiasi cha kujiona duni kwa hili na
lile na wakati mwingine hali hiyo humfanya ashinde kufanya hata mambo ambayo
anayajua na kwamba amekuwa akiyafanya kila siku
Kisaikolojia huu ni ugonjwa ambao unaweza
kuathiri uwezo wa mtu kibaiolojia, nikimaanisha kwamba mtu anaweza kuwa si
mlemavu wa miguu, lakini akatembea mbele za watu upande upande, anaweza kuwa na
akili lakini akajikuta hawezi kuzitumia kwa sababu si mwenye kujiamini.
Kama ilivyo kwa magonjwa mengine, kuponywa kwa tiba,
tatizo hili la kutokujiamini nalo linatakiwa litibiwa. Zipo njia nyingi ambazo
mtu anaweza kuzitumia kujenga hali ya kujiamini, Kwangu mimi yako mambo 10 ya msingi ambayo mtu akiyazingatia
na kuyafanyia kazi anaweza kuondokana na hali ya kutokujiamini.
Kuchagua mavazi
Ingawa mavazi hayatafsiri moja kwa moja
hali ya mtu, lakini katika lugha ya mawasiliano yasiyokuwa na sauti uvaaji wa
mtu ni utambulisho wake. Hivyo kama mtu hazingatii uvaaji unaokubalika katika
jamii anakuwa katika wakati mgumu wa kujiamini, hasa kama
akilini mwaka yeye mweyewe atatambua kuwa amevaa vibaya.
Hii ina maana kwamba kama
mtu anataka kujenga hali ya kujiamini, lazima achague mavazi yanayoendana na
mazingira na yawe ni mavazi ambayo mwenyewe akiyafikiria yahatamfanya ajione ni
wa tofauti kwa wenzake. Mavazi hujenga muonekano, ukionekana vizuri mbele za
watu utajiamini, hivyo kuwa makini na uchaguzi wa mishono ya nguo unazovaa kila
siku.
Kutembea haraka
Njia rahisi ambayo imethibitika kuweza
kumuondolea mtu hali ya kutokujiamini ni kutembea kwa mwendo wa haraka.
Haipendezi unapokuwa njiani kutembea kama mgonjwa,
uliyechoka. Ukiwa hivyo ni rahisi sana
kuwafanya watu wakukodolee macho ambayo yatakufanya wewe uhisi tofauti.
Utemebeaji wa haraka una faida nyingi, lakini kubwa kabisa ni kuwafanya watu
wengine wakuone wewe ni mtu wa kazi usiyetaka kupoteza muda wako, mtu makini na
mwenye mipamgo. Kitaalamu mwendo unaoruhusiwa ni wa asilimia 25, usizidi sana kiasi cha kuonekana kama
unakimbia.
Muonekano sahihi
Namna mtu mwenyewe anavyouweka mwili wake
linaweza kuwa ni tatizo la kumfanya ashindwe kujiamni. Kwa mfano,mtu kama si mlemavu
lakini akajikuta anatembea miguu upande, mabega juu, kichwa chini au juu sana au kutembea akiwa anadundika kama
mpira, ni vibaya kwa vile kitalaamu huchangia kumuondolea mtu ujasiri mbele za
watu.
Ushauri wangu ni kwamba mtu anatakiwa
kuupa mwili wake umuhimu na kuuweka kama
alivyoumbwa, haifai kuwa mtu wa kuinama na kuficha uso, kusimama tenge pale
unapoitwa au kuwa mbele za watu. Si vema pia kung�ata kucha, kujipapasa mwilini
au kutazama pembeni. Ni vizuri kila mtu kulinda muonekano wake wa asili mbele
za wenzake.
Kujizoeza kujiamini
Njia moja muhimu sana kisaikolojia ya kujenga hali ya
kujiamini ni kupenda kusikiliza maneno ya kutia moyo nay a ujasiri kutoka kwa
watu maarufu. Kwa mfano, viongozi wenye msimamo, watetezi wa haki za binadamu,
wanasiasa wanaotetea maslahi ya nchi bila hofu na kadhalika. Hotuba na maneno yao yakipata sehemu kubwa katika akili ya mtu, lazima
yatajenga hali ya kujiamini kama wale anaowasikiliza.
Kukubali matokeo
Ifahamike kuwa ukiwaza kwa kina sana juu ya mahitaji yako,
zao litakalofuata hapo ni akili kukuletea sababu za kishindwa kufanikisha mambo
unayoyataka. Sababu hizo ukizipa nguvu sana
ya kuziwaza zitakupa jibu la haiwezekani. Unapokuwa na mawazo yenye mlango huo
wa kutokufanikiwa, uwezo wako wa kujiamini hushuka na kujikuta unashindwa
katika mambo uyafanyayo. Katika maisha lazima mtu akawa na wakati wa kuachia
mawazo yake na kukubaliana na matokeo yaliyopo hasa pale hali ya kushindwa
inapokuwa kubwa.
Kupingana na wengine
Mtu akijiona duni mwenyewe ni rahisi
kwake kudhani kuwa watu wengine ndiyo wenye mambo ya kweli na hivyo kujikuta
akifuata mkumbo na kupotoshwa katika ukweli. Ili
mtu aweze kuwa sahihi katika mawazo ya vile ananvyoamini ni lazima awe na tabia
ya kupingana na wenzake. Ni jambo baya kukubaliana na watu katika mawazo yao bila kupinga katika
kile unachoamini, kufanya hivyo kunaweza kuyafanya maneno ya uongo ya wengine
yakaaminika na kuuacha ukweli wa mtu asiyejiamini ukipuuzwa kwa sababu tu
hakuwa na ujasiri wa kukabiliana na hoja za wenzake.
7. Pendelea kukaa mbele
Katika kujenga hali ya kujiamini ni vizuri zaidi unapokuwa shule, ofisini, kwenye mikutano, semina ukawa na tabia ya kuketi nafasi za mbele. Ni ukweli kuwa, watu wengi hawapendi kukaa sehemu za mbele kwa sababu ya hofu ya kuonekana kwa urahisi na pengine kuwa wa kwanza kuulizwa au kuchangia hoja, tabia hiyo huondoa hali ya mtu kujiamini. Ili kujenga ujasiri ni vema mtu akapendelea kuketi vitu vya mbele na mara nyingi kuwa wa kwanza katika kufanya mambo.
Katika kujenga hali ya kujiamini ni vizuri zaidi unapokuwa shule, ofisini, kwenye mikutano, semina ukawa na tabia ya kuketi nafasi za mbele. Ni ukweli kuwa, watu wengi hawapendi kukaa sehemu za mbele kwa sababu ya hofu ya kuonekana kwa urahisi na pengine kuwa wa kwanza kuulizwa au kuchangia hoja, tabia hiyo huondoa hali ya mtu kujiamini. Ili kujenga ujasiri ni vema mtu akapendelea kuketi vitu vya mbele na mara nyingi kuwa wa kwanza katika kufanya mambo.
Zungumza bila aibu
Ukimya wa kupita kiasi nao ni tatizo,
hasa pale linapokuja suala la kuogopa kuzungumza mbele za watu kwa hofu ya
kuonekana hujui. Wapo wanafunzi na wasomo wengi wanapokutana katika vikundi vya
mazungumzo maarufu kama Groups Discusions huwa
hawapendi kuzungumza wakilenga kujificha na aibu itokanayo na udhaifu wao katika
uelewa. Hata hivyo kutochangia mazungumzo na wengine hakuna faida zaidi ya
hasara kwa mtu kutoweza kujiamini. Inashauriwa kwamba ili mtu aweze kujenga
hali ya kujiamini ni vema akajenga mazoea ya kuongea mbele za watu bila aibu.
Kujenga afya
Kipengele cha kulinda afya ni muhimu sana kwa mtu anayetaka
kujenga hali ya kujiamini. Kukonda au kunenepa sana umbo kunaweza kumfanya mtu akajiona wa
tofauti na hivyo kupoteza hali ya kujiamini. Hivyo basi kama unakonda hakikisha
kuwa unakula vyakula vyenye vitamini ili kuufanya mwili wako usiwe kituko kwa
wengine, hali kadhalika kama unanenepa sana
fanya mazoezi ili kuupunguza mwili wako. Tafuta afya ili uwe na nguvu za
kufanya mambo kwa umakini.
Msaada kwa wengine
Baada ya kufanikiwa katika hatua zote
ambazo tumeziangalia hapo juu, jambo jingine la muhimu katika kuhitimisha uwezo
wa mtu kujiamini ni kupata msaada wa mawazo kutoka wa watu wengine ambao ni
makini katika maisha yao.
Kama kuna jambo ambalo linakuwa gumu katika
mawazo yako na limekosa ufumbuzi kiasi cha kukufanya usijiamini, washirikishe
wengine wakusaidie na kukutia moyo wa
kuendelea kukabiliana na hali yakutojiamini.
No comments:
Post a Comment