NJOMBE

NJOMBE

Saturday, October 6, 2012

12,000 wafutwa kazi kwa kugoma A.Kusini

Wachimba migodi wa Amplats waliofutwa kazi
Kampuni kubwa zaidi duniani ya madini ya Platinum, Anglo American Platinum, imewaachisha kazi wachimba migodi 12,000 waliokuwa wanagoma kudai nyongeza ya mishahara.
Kampuni hiyo, Amplats, ilisema kuwa mgomo haramu wa wiki tatu uliofanywa na takriban wachimba migodi 28,000 mjini Rustenburg, uliiletea hasara ya dola milioni 82.3.
Sekta ya madini nchini Afrika Kusini, imekumbwa na migomo ya wachimba migodi na hata kukatokea maafa baada ya polisi kuwapiga risasi zaidi ya wachimba migodi 30, waliokuwa wanagoma kutaka waongezwe mishahara.
Ikieleza sababu ya kuchukua hatua hiyo, Amplats, ilidokeza kuwa, wachimba migodi walikosa kuhudhuria vikao vya kinidhamu na ndiyo maana wakaachishwa kazi.
Kwa kukosa kuhudhuria vikao hivyo ilimaanisha kuwa shughuli za kuchimba madini hazingefanyika ipasavyo
Wafanyakazi walielezwa matokeo ya vikao hivyo hii leo na walikuwa na siku tatu kukata rufaa.
Takriban wachimba migodi 12,000 waliamua kutohudhuria vikao hivyo. Na kwa hivyo wakaachishwa kazi bila kuwepo wenyewe.

No comments:

Post a Comment