Baraza la usalama
la Umoja wa mataifa, limeshutumu mashambulizi ya roketi yaliyofanywa na
Syria katika mji wa mpakani nchini Uturuki ambapo watu watano waliuawa.
Baraza hilo limetoa onyo kwa Syria kukomesha
mashambulizi kama hayo, yanayokiuka sheria za kimataifa na kuitaka
iheshimu uhuru na mipaka za jirani zake.Urusi ilikataa kuunga mkono kielelezo cha awali cha azimio hilo kilichotaja shambulizi hilo kama tisho kwa amani na usalama wa kimataifa kwa sababu ya maandiko yake.
Bunge la Uturuki, limeidhinisha hatua za kijeshi dhidi ya Syria, hatua ambayo ilichochea maandamano ya kupinga vita.
Hata hivyo, waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa nchi yake haina nia ya kuanza vita dhidi ya Syria.
Balozi wa Syria katika Umoja wa mataifa alisema kuwa nchi yake, ilitoa pole zake kwa shambulizi hilo ambalo lilisabaisha vifo, lakini haikuomba radhi kwani uchunguzi ungali unaendelea.
No comments:
Post a Comment