NJOMBE

NJOMBE

Friday, October 19, 2012

Guinea yaruhusu silaha kuingizwa Mali

Jeshi la Mali lilipindua serikali na kuishtumu serikali kwa kutochukua hatua kali dhidi ya waasi
Serikali ya Guinea imeruhusu silaha zilizokuwa zinapelekwa nchini Mali kupitia nchini humo, kuweza kukabidhiwa Mali baada ya kuzizuilia kwa muda kwa sababu ya tisho la usalama nchini Mali.
Shirika la nchi za ukanda wa Magharibi, Ecowas, ambalo limekuwa likitatua mgogoro wa kisiasa nchini humo, lilichunguza silaha hizo zilizokuwa zimebebwa kwa Meli kuidhinisha ziingizwe Mali.
Zana hizo zinatoka nchini Bulgeria na zimepitishiwa Guinea kwani Mali haina bandari.
Mwandishi wa BBC Alhassan Sillah, mjini Conakry, anasema kuwa habari za kuzuiliwa kwa meli hiyo zilitolewa mwezi Agosti, na kwamba hakuna taarifa rasmi imetolewa kuhusu silaha hizo.
Kumekuwa na mikutano kadhaa kutoka Mali na shirika la Ecowas kuamua hatua za kuchukua kuhusiana na silaha hizo.
Shirikia la habari la AP lilimnukuu waziri wa ulinzi wa Guinea Abdoul Kabele Camara, akisema kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba vifaru, magari za kivita na sialaha nzito.
"Ecowas lilifika hapa kubaini kilichokuwa ndani ya meli hiyo na kwa pamoja tukaamua kuwa tutairuhusu kupiitisha silaha hizo. Sasa hivi tunasubiri serikali ya Mali ijiandae namna itakavyo safirisha silaha hizi kutoka hapa'' alisema bwana Camara
Jeshi la Mali lilitwaa mamlaka mwezi jana kabla ya uchaguzi mkuu likishtumu aliyekuwa rais Toure, kwa kukosa kukabiliana vilivyo na waasi wa Tuareg, lakini waasi hao baadaye walitumia nafasi ya mapinduzi hayo kuzua ghasia na kudhibiti miji kadhaa ya eneo la Kaskazini.

No comments:

Post a Comment