Pombe,Sigara Na Ukahaba Marufuku Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku biashara ya ukahaba, matangazo
yote ya pombe na uvutaji wa sigara katika mikusanyiko ya watu katika
visiwa vya Unguja.
Hayo yamebainika kufuatia marekebisho ya kifungu cha sheria cha 112, cha
mswada wa sheria kuhusiana na hifadhi na usimamizi wa vihatarishi vya
afya ya jamii na afya
ya mazingira na mambo yanayohusiana na hayo iliyopitishwa ndani ya
Baraza la Wawakilishi jana.Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji
aliwaambia wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba kutokana na michango
mingi ya wajumbe kutaka suala la matangazo ya pombe, uvutaji wa sigara,
na biashara ya ukahaba vipigwe marufuku, serikali imekubaliana na maoni
ya wajumbe hao. Waziri Duni amesema, kuanzia sasa kwa mujibu wa sheria
hiyo itakuwa ni marufuku kutangaza au kushajiisha matangazo ya pombe kwa
kutumia njia mbalimbali zikiwemo ufadhili au matamasha ya muziki na
starehe katika visiwa hivyo. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud
Othman alisema anakubaliana na maoni ya wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi kuondoa kabisa matangazo ya pombe na kwamba serikali
imefanya vyema, kwani hivi sasa Shirika la Afya Duniani WHO, Umoja wa
Ulaya EU na baadhi ya nchi ikiwemo Sweden tayari zimezuia matangazo ya
pombe na Zanzibar kufuata sheria hiyo ni jambo la busara.
No comments:
Post a Comment