Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Temeke David Misime ameiambia Wapo Radio Fm kuwa licha ya kuwashikilia watu hao bado wanaendelea kufanya msako wa kuwakamata watu wengine zaidi kutokana na tukio hilo la uvunjifu amani. Mpaka sasa makanisa yamepata uharibifu kutokana na tukio hilo ambayo ni Kanisa la Assemblies of God, Lutheran, Wasabato, Anglican yote ya maeneo hayo ambako vioo milangoni vilivunjwa, gari kuchomwa, vyombo kuharibiwa na kuchomwa moto.
Kwa upande wa sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhaji Musa Salum amewataka viongozi kutoka misikiti yote jijini kuwaeleza waumini wao kutopandikiza chuki kwa dini nyingine hali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa,'' Wakristo wasihukumiwe kutokana na tukio hilo, kwani aliyefanya hivyo ni mtoto akiwa katika utani na mwenzake ...hajatumwa na kanisa, ni watoto waliofanya hivyo na jazba isiwepo kabisa'', alisema sheikh Salum.
Hamis Salum baba mzazi wa kijana aliyekojolea kitabu hicho |
Moja ya gari lililovunjwa kioo. |
Chanzo cha Habari Gospel Kitaa |
No comments:
Post a Comment