MSANII Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi
kuwa kifo cha
Steven Kanumba kimetokana na ugonvi kati yao, huku taarifa nyingine
zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo.
Habari
zilizopatikana jana kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa,
Lulu alisema kuwa kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye
kuzungumza na simu
kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake.
"Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo
Kanumba akamfokea na ndiyo ugomvi ukaanzia hapo," chanzo hicho kimesema.
Chanzo
hicho kiliongeza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje na
kuondoka kwa gari lake hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari
wa Kanumba alimpigia simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali.
"Alipororudi Sinza ndipo akakamatwa, lakini walikuja Kituo cha Polisi Oysterbay kuchukua PF3," kilisema chanzo hicho.
Chanzo
kiliongeza kuwa tangu Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivu
asiye na wasiwasi wowote hata katika mahojiano na polisi.
Katika
hatua nyingine, Polisi wa kituo hicho jana walipata wakati mgumu baada
ya kuibuka kundi la vijana waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika
Kanumba, walioandamana wakidai wanamtaka Lulu.
"Tunataka jembe
letu", waliimba vijana hao waliofikia 100 wakitokea Barabara ya Ali
Hassan Mwinyi huku wakishika majani na kufanya askari waliokuwapo
kituoni hapo kuwahi kuchukua silaha na mabomu ya machozi kujiandaa
kutuliza ghasia kama zingezuka.
Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayari kupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa,
Msanii
Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu huenda akafikishwa
mahakamani leo kujibu tuhuma za kuhusika na kifo cha Steven Kanumba.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliliambia gazeti hili
jana kuwa Lulu atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni
mara baada ya polisi kupata ripoti ya vipimo kutoka Mkemea mkuu wa
Serikali.
“Tunasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu kubaini chanzo cha
kifo hicho kwa sababu wamechukua baadhi ya sampuli za marehemu kwenda
kupima na kwamba tutakabidhiwa leo(jana). Kimsingi tukipata tu taarifa
hiyo tutamfikisha mahakamani,” alisema Kenyela.
Aliongeza ripoti
hiyo itaweza kuwasaidia kuandika mashtaka ili yaweze kufikishwa kwa
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.
Kamanda
Kenyela alisema kuwa, ripoti ya madaktari imewasilishwa juzi na kwamba
imeonyesha kuwa Kanumba amefariki kwa ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo.
Msanii Stephen Kanumba alifariki usiku wa Ijumaa Kuu
Chanzo Mwananchi.
No comments:
Post a Comment