Wateja wakubwa wa mapipa laki
mia moja na themanini ya mafuta yanayoibwa kutoka nchini Nigeria wako
katika nchi za Kusini Mashariki mwa Ulaya pamoja na Singapore, kulingana
na wanaharakati.
Mwanasiasa kutoka jimbo lenye utajiri wa mafuta
la Niger Delta, Patrick Dele Cole, amesema kuwa asilimia tisini ya
mafuta yanayoibwa yanasafirishwa kwenda nje ya nchi kinyume na sheria.Nigeria ni mojawapo ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi ingawa idadi kubwa ya wananchi wake wanaishi kwa umaskini
Kampeini hiyo inalenga kuzichunguza meli hizo kwa satelite na kubaini pesa zinazotokana na uuzaji huo zinakokwenda.
''Unapoanza kuuliza maswali, na kuanza kuangazia swala hili, utakuwa umesuluhisha zaidi ya asilimia hamsini ya matatizo kuhusiana na wizi wa mafuta.'' alisema bwana Dele Cole, mwanadiplomasia mkongwe na mshauri wa zamani wa rais.
''Nadhani ni mumimu kutoa onyo kwa wale matajiri kwamba siku yao ya kuwajibika itafika''
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa sekta nzima ya mafuta nchini humo inakumbwa na ufisadi,
Wanasiasa wengi wanahusika na wizi huo anasema Will, huku sehemu ya mapato ya mafuta hayo yakitumiwa kununua kura na kufadhili kampeini zao.
Jeshi la Nigeria linapaswa kusitisha visa vya wizi wa mafuta lakini wao huchukua hongo ili kutofuatialia visa hivyo
No comments:
Post a Comment