Waakilishi wa kampuni kubwa ya
mafuta ya Shell, wamefika mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya
kuchafua mazingira nchini Nigeria.
Wakulima wanne kutoka eneo lililo na utajiri
mkubwa wa mafuta la Niger Delta nchini Nigeria leo wameifikisha Kampuni
hiyo kubwa ya mafuta ya Shell katika mahakama ya kimataifa ya uholanzi
kujibu madai ya uchafuzi wa mzingira katika vijiji vinne nchini Nigeria.Wakulima hao wanasema uvujaji wa mabomba ya mafuta yanayomilikiwa na kampuni hiyo yameharibu mashamba yao na biashara ya samaki.
Wa-Nigeria hao wakiungwa mkono na wanaharakati wa mazingira kutoka Uholanzi wanataka Kampuni ya Shell ilazimishwe kusafisha mazingira na kulipa fidia kwa hasara iliyotokea huko Niger Delta.
Kesi hiyo imewasilishwa mahakamani na wakulima wanne wa Nigeria kwa ushirikiano na shirika moja la kutetea mazingira la nchini humo, Friends of the Earth.
Ni mara ya kwanza kwa kampuni kubwa ya Uholanzi inashtakiwa katika mahakama ya kiraia nchini humo kuhusiana na uharibifu uliotokea katika nchi ya kigeni.
Shell, inasisitiza kuwa haijaweza kusafisha eneo ambalo lilichafuka kutokana na shughuli zake nchini Nigeria.
Inasemekana kuwa nusu ya uvujaji wa mafuta katika eneo hilo umesababishwa na visa vya wizi.
Kesi hiyo inahusishwa na uvujaji wa mafuta uliotokea katika eneo la Ogoniland nchini Nigeria.
Wakulima wanasema kuwa mafuta yaliyovuja kutoka kwa mabomba ya mafuta ya kampuni hiyo, yameathiri mapato yao, kwa kuharibu mimea na mabwawa ya samaki.
Mmoja wa walioshtaki kampuni hiyo, Alfred Akpan, aliambia BBC kuwa mafuta yaliyovuja yaliharibu vibaya mabwawa yake 47 ya samaki na anataka fidia.
No comments:
Post a Comment