NJOMBE

NJOMBE

Saturday, October 20, 2012

Benki za Ulaya kuwekewa sheria


Viongozi wa ulaya wamepiga hatua kukaribia kuziweka benki elfu sita za nchi za Jumuiya ya Ulaya chini ya udhibiti wa chombo kimoja cha usimamiaji.
Mpango huo ulitangazwa katika mkutano wa nchi za Jumuiya ya Ulaya mjini Brussels, huku chombo hicho cha usimamizi kikitarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka ujao.
Inaonekana ni makubaliano kati ya Ufaransa na Ujerumani ambazo awali zilipingana juu ya muda na idadi ya benki chombo hicho kimoja kitachozisimamia.
Akizungumza katika mkutano huo rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema ni jambo muhimu kuwa wameafikiana tarehe maalum kuhakikisha mfumo wa sheria unawekwa kwa ajili ya mpango huo.
Bwana Hollande pia amesema kazi zaidi inahitajika kufanyika kabla chombo cha usimamizi hakijaanza kutoa msaada kwa mabenki hapo mwaka kesho.

No comments:

Post a Comment