NJOMBE

NJOMBE

Saturday, October 13, 2012

HIVI NDIVYO MBAGALA ILIVYOKUA JANA MCHANA KUTWA! Mtoto wa Form one asababisha madhara makubwa, Ni baada ya kukojolea Quraan na kumdunda mtoto wa madrassa.

Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha FFU wakiruka mtaro na watuhumiwa wavurugu zilizo zuka jana kwenye eneo la Mbagara Kizuiani, baada ya mtoto anaedaiwa kuwa wa kidato cha kwanza kudaiwa kukojolea mkojo Qurani na kusababisha taharuki kubwa mchana wote wa jana ambapo hadi sasaivi hapa Mbagala bado kuna Vurugu.

Baadhi ya watu waliokuwa na shughulizao kwenye eneo hilo walishindwa kabisa kuendeleanazo kufuatia vurugu hizo. Mama huyu pichani alikua anatoka msikitini kusali sala ya Ijumaa lakini akakutana na dhahama ya mabomu na kulazimika kukimbia.
Baadhi ya vijana wanaodaiwa kuendesha vurugu hizo wakipandishwa kwenye gari la polisi eneo la Kizuiani.
Hapa hawajamaa waliona vijana waliovalia kanzu kando ya barabara wakaanza kuwafukuzuia alama kuu ya askari ili kukukamata kwanza ilikua kanzu pili sijida kwenye paji la uso ukikatiza tu usalimiki lazima watakutia nguvuni.
Hapa waisilamu hao waliwakomalia polisi kazi ikawa piga nikupige uso kwa uso bila kulimbikizia na mabom basi virungu vingeshindwa maana walikua na nguvu kwelikweli wakitaka kuvamia kituo cha polisi cha Maturubai kwenye eneo hilo la Kizuiani.
Wateule wachache wakatiwa nguvuni huku wakila kisago cha nguvu kutoka kwa askari hao.
Hawa ni baadhi ya vijana waliokamatwa kwenye Chochoro mbalimbali za eneo hilo baada ya kukimbia mabomu na kujificha.

Kimbembe kilikua hapa hawa jamaa wanaokula virungu ni wale walioamua kukaa chini na kuwaambia askari pigeni mtakavyo hatutoki.
Baadhi ya wananchi wakazi wa eneo hilo wakilalamikia mabomu na kudai yanawaumiza sana kwani kwa mchana kutwa waleo hali ni mbaya kunawatoto wengine wamelazwa.
Hili ni moja kati ya makanisa matatu yaliyovunjwa, hapa baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia vioo vilivyovunjwa kwenye Kanisa hilo Jipya la Wasabato lililopo upande wa magharibi mwa karibu na kituo cha mabasi kizuiani.
Barabara zilifungwa kwa mawe na askari kupata wakati mgumu kupita.
Barabara zilizuiwa na matariri yaliyochomwa moto

Vijana wa umri huu ndio walikuwa wakiwahenyesha polisi kwa muda wote kwani ni wajanja na wanambio.



Mtuhumiowa akipandishwa kutoka kwenye mtaro kuelekea kwenye gari.

No comments:

Post a Comment