Mahakama kuu nchini
Uingereza leo inatarajiwa kutoa uamuzi wake katika kesi iliyowasilishwa
na mashujaa watatu waliopigania uhuru nchini Kenya ,Mau Mau, dhidi ya
serikali ya nchi hiyo.
Wakenya hao wanadai waliteswa na kudhulumiwa na
serikali ya ukoloni ya Uingereza katika miaka ya 1950, wakati wa
harakati za kupigania uhuru wa taifa hilo.Mahakama hata hivyo itaamua ikiwa kesi itaendelea au iamrishe walipwe fidia.
Lakini mawakili wa serikali watakuwa wanateta wakisema kuwa kesi ya haki haiwezi kutendeka kwa sababu matukio hayo yalitokea miaka ya hamsini.
Mapema mwaka huu, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Askofu mkuu mstaafu Desmond Tutu, alimtumia ujumbe waziri mkuu David Cameron akimtuhumu kwa kujaribu kukwepa kuwajibika kisheria kwa makosa yaliyofanywa na wakoloni.
No comments:
Post a Comment