Chansela wa Ujerumani Angela
Merkel, ametoa wito kwa Muungano wa Ulaya kuwezesha nchi wanachama kuwa
na haki ya kuhoji bajeti ya taifa za nchi wanachama wengine
Bi Markel aliyasema hayo kwenye mkutano wa
vingozi wa ukanda huo, waliokutana mjini Brussels kutafuta mikakati ya
kumaliza msukosuko wa kifedha barani Ulaya.Ufaransa na Uhispania, zinataka mfumo mpya kuanza kutumika kuanzia Januari, tarehe mosi.
Uingereza ambayo ndiyo kitovu cha fedha barani Ulaya, inataka sheria zitakazoweza kulinda benki ya Uingereza.
Bi Merkel aliunga mkono wito wa waziri wake wa fedha Wolfgang Schaeuble, wa kutaka kamishna wa kusimamia sarafu ya Ulaya ambaye jukumu lake litakuwa kupiga kura ya turufu dhidi ya bajeti za nchi wanachama ikiwa zitavunja sheria za sarafu.
No comments:
Post a Comment