Habari
za leo tena natumai sote tu wazima ,si lengo langu kuwa beza wale walio
vitandani na ma hosptalini wakijiuguza au kuugulia hapana, amani na
uponyaji uwe juu yao. Nifuraha yangu kukutana tena leo katika UKURASA
huu, lengo na dhumuni langu ni kuzungumzia mambo machache kuhusu maisha ya vijana na mahusiano ya kimapenzi.
Kwangu mimi, ni kitu ambacho nakiamini kwa mtazamo wangu na ningeomba sote tukichukulie kama angalizo tu kwa kile ambacho nita kiongelea hapa.
Kumekuwa
na matukio mengi katika mahusiano ya vijana na hata watu wazima ,lakini
ningependa kutumia nafasi hii kuzungumzia sana vijana wa rika kama
langu(miaka 18-35). Katika kipindi cha karibu kumekuwa na wimbi kubwa la
vijana wadogo kujikita katika dibwi la mahusiano katka umri ambao ni
mdogo na hiii imepelakea dunia ya maraha kuwa na vita baridi kwa vijana,
ambavyo wengi wetu tumekuwa hatumjui adui yetu hasa katika vita hii,
nikinukuu kauli ya kiongozi mmoja wa zamani wa jamhuri ya china alisema “....hakuna wakati mzuri katika kipindi cha vita kama mwisho wa vita hiyo....““
Katika
asiimia 100 ya vijana walio katika mahusiano ya kimapenzi ni kwa
asilimia 25 tu ndio kwa hakika wanafuraha ya kweli katika mahusiano yao,
kwa mtazamo wangu.
Zifuatavyo ni sababu ya zinatuweka vijana katika wakati mgumu kimahusiano.
1. 1. Utandawazi
2. 2. Kutosoma nyakati
3. 3. Uelewa mdogo wa nini na nani chaguo lako
utandawazi
kutokana
na ukuaji wa teknologia na sayansi, hali hii imeathiri kwa kiasi
kikubwa mahusiano ya vijana katika jamii yetu kwa sasa, vijana wengi
tumekuwa ni watu wa kuishi katika jamiii nyingine au tamaduni nyingine
katika nyanja ya kimahusiano.,tumekuwa ni watu wa kuiga na kuishi
kitamthilia zaidi, na shawishika kusema tunaishi kivenezuela na
kifilipino zaidi.
Anyway ni vizuri kujua na
kufahamu nini tamaduni na mila za watu wengine , lakini limeibuka
tatizo la vijana wengi kutaka kuishi maisha tofauti na tamaduni zetu
hilo limepelekea vijana wengi kushindwa kuelewa nini na kwa muda gani vitu hivi vifanyike na kushindwa kuvichukulia vitu kwa ukubwa wake.
Ushauri
wangu ni vema vijana tuishi kati yetu wenyewe (yaani katika tamaduni na
mazingira yetu)hii itapunguza kwa kiasi kikubwa maumivu na misukosuko
miongoni mwetu. Watafsiri wa mambo wanasema ni vema kuishi kama wewe
kwani ukishi kama mwingine, hakuna wa kutimiza majukumu yako katika nafasi yako kama wewe ..hivyo ilo litakuwa ni tatizo ambalo mtatuzi ni wewe. So be yourself no matter how is hard to be...
Nyakati
Ni
kweli mambo yanakwenda yakibadilika na mabadilio kwa binadamu ni kitu
ambacho ni vigumu kikizuia, lakini pia sio kila kitu kina badalika au
kinaendana na mabadilko hayo, vingine vilikuwepo vipo na vitaendelea
kuwepo tu bila kujali kigezo cha muda au Nyakati. Ni vema tukaliangalia
upya swala ili la mabadilko na mahausiano. Kama nilivyosema mwanzo sasa
kumekuwa na lundo la vijana wadogo kujiingiza katika mausiano katika
umri mdogo, pasipo kuwa na utayari na ukomavu wa akili na kiuchambuzi
pia.
Ushauri wangu ni
vema jamii kwa ujumla kukaa na kulizungumzia jambo hili kwa upana na
ukubwa wake pasipo kujali rika ili kuweza kukinusuru kizazi hiki cha
sasa. Its better to be open for the best direction
Uelewa mdogo
Hili
nitatizo pia kwa upande wake , si tu kujua nini mwenzi wako anapenda na
nini hapendi lakini nadhani ni zaidi ya kujamiana,(ngono) mapenzi ni
uwanja mpana sana ambao wausika wanahitaji kuwa na uelewa mpana wa
kutambua mipaka ya upana huo ili kuweza kuwa na ufanisi mkubwa katika
kulitumia jukwaa hilola wapendana nao…
Kwa leo naomba niishie hapa…..
Lakini kuna mengi ya kuyazungumzia na kuchangia pia,nijukumu letu sote kusaidiana na kushauriana pale inapowezekana pia….. kwani kujua bila kufanya siyo kujua(to know without doing is not knowing)
No comments:
Post a Comment