Mashirika ya
kutoa misaada nchini Niger yamesema kuwa takriban wafanyakazi wanne wa
mashirika hayo wametekwa nyara na watu wasiojulikana na ambao walikuwa
wamejihami.
Wafanyakazi hao kutoka Niger na Chad walitekwa
nyara wakiwa mjini Dakro ambako walikuwa wakitibu wagonjwa wa Malaria na
kuwasaidia watoto wanaokumbwa na utapia mlo.Serikali ya Niger, imetuma wanajeshi kuwatafuta wafanyakzi hao.
Hata hiovyo haijulikani nani au kundi gani limefanya kitendo hicho.
Makundi ya kigaidi yenye uhusiano na Al Qaeda yamekuwa yakilaumiwa kwa visa vya awali vya utekaji nyara nchini Niger
No comments:
Post a Comment