NJOMBE

NJOMBE

Friday, October 19, 2012

PENGO KATI YA MATAJIRI NA MASIKINI KAMWE HALITOPUNGUA IKIWA SEKTA YA ELIMU HAITAPEWA KIPAUMBELE KWA MIZANIA SAWA.

Leo hii tunaona shule ambazo zimeboreshwa na kuwa na kila kitu kinachohitajika ili kumfanya mwanafunzi aweze kujifunza na kuelewa vizuri lakini unaona ni za gharama sana hivyo kwa watu wa kipato cha chini kutoweza kumudu kuwasomesha watoto wao huko. Hivyo shule hizi zimekuwa ni kwaajili ya watoto wa matajiri tu.
Shule ambazo watu wakipato cha chini wanamudu kusoma ni zile za serikali ambazo zimezorota kabisa! hakuna vitendea kazi kwa walimu, madawati kwa wanafunzi, upungufu wa vyumba vya madarasa na hivyo kufanywa wanafunzi kusomea nje tena mchangani, walimu wachache nk. Shule hizi zimejaa kila aina ya changamoto. Si rahisi hata kidogo kutegemea mipango endelevu ya maendeleo ya taifa tuliyonayo kutimia ikiwa shule hizi ambazo Watanzania wengi wanazitumia hazitoboreshwa.
Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi sana, hivi serikali inazio
na shule hizi? au kwa vile watoto wao hawasomi shule hizi ndo maana wanafumbia macho. Kwa nchi hii iliyojaa utajiri ni ajabu kweli kuona hali hii. Wageni wanakuja hapa na kuondoka na mabilioni ya mali zenu huku wananchi wakiachwa fukara wa kupindukia. Km huamini tembelea migodi ya dhahabu na madini mengineyo, nenda kule mnazi bay uone wale wageni wanavyotanua ktk nchi yetu. Wakati mtu unawaza namna ya kufika kazini kwa daladala ukiwaza karaha za foleni wenzio wanaishi Dar na kufanya kazi Mtwara, kila siku wanatoka na ndege Dar na kuingia Mtwara na jioni kurudi. Hata siku moja hatujiulizi ukubwa huu wa gharama hizi za uendeshaji kama zinatupa picha ya thamani ya madini tuliyonayo!!! Madini yananchimbwa na yanapakiwa ktk ndege zao kupelekwa nchini kwao pasipo hata serikali kujua.
Serikali iweka utaratibu ambao utasaidia taifa kupata maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizopo. Ndiyo hatuna mitambo ya kuchimbia rasilimali hizi lakini haina maana kwamba tuwaachie. Ipo haja ya serikali kuingia mikataba ya kuchimba hizi rasilimali na uuzaji wake uwe chini ya serikali na makampuni yanayochimba. Serikali isimamie moja kwa moja migodini na kuidhinisha kiasi chote kinachochimba na kukuchukua kisha kukiuza kule ambako thamani yake ni kubwa na ina tija kwa Taifa letu. Makapuni yanayochimba yabaki kulipwa pesa kwa kazi yao ya uchimbaji tu ni si kama ilivyo sasa hivi.

No comments:

Post a Comment